Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 19, 2013

YATOKANAYO NA KIKAO CHA KAMANDA KOVA, KENYELA NA KIONDO KUHUSU MAKAHABA



HATIMAYE malumbano yaliyokuwa yakiendelea kati ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, yamekwisha baada ya kupatanishwa.

Malumbano hayo, yaliibuka baada ya Kamanda Kenyela kuendesha operesheni ya kuwakamata wanawake wanaojiuza (changudoa, CD, mahakaba), kitendo ambacho kilipingwa vikali na Kamanda Kiondo, kwa kile alichokidai hakuna sheria inayowazuia kujiuza.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema mzozo huo ulimalizwa katika kikao kilichoketi juzi na kuwajumuisha maofisa wa polisi ngazi za juu kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi.

Kikao kilikuwa cha moto kwa sababu kiliwajumuisha maofisa wakubwa kutoka makao makuu na kila mmoja alijieleza kwa nafasi yake, lakini tulichobaini ni kwamba wote walikuwa sahihi, walitofautiana katika tafsiri ya utendaji kazi.

Sisi kama polisi, kuwakamata wale makahaba na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ni sahihi kama alivyofanya Kamanda Kenyela, lakini pia kuwapa elimu bila kuwafikisha mahakamani ni njia sahihi kama alivyosema Kamanda Kiondo.


Tatizo, inategemea makahaba hao wapo katika mazingira gani na jinsi gani wanavyofanya vitendo hivyo ili kuepuka kubughudhi watu wengine… polisi tuna utaalamu wa kubaini hapa wanavunja maadili ya jamii au la.

Kwa ujumla, tumewaonya makamanda wote wawili na wakakiri kwamba wameondoa kinyongo walichokuwa nacho dhidi ya mwingine, lakini kubwa tulitoa wito kwa makamanda wengine kuchukua tukio hilo kama changamoto kwao na kuliepuka.

Tumetoa wito kwa makamanda wote nchini, hatutegemei tena kusikia malumbano yakiibuka kutokana na kukosoana kwenye utendaji ndani ya Jeshi la Polisi.
Alisema makamanda wote wa Kanda Maalum, wameagizwa kudhibiti vitendo hivyo kwa njia mbili, ya elimu na sheria, ili kurudisha maadili ndani ya jamii kwa kuwa vinaonekana kushamiri na kufanyika hadharani.

Awali Kamanda Kiondo, alisema operesheni ya Kamanda Kenyela aliifanya kwa kukurupuka kutokana na kutokuwa na elimu ya jamii, yaani sociology.

Alisema hakuna sheria inayowazuia wanawake kujiuza na kuongeza kitendo cha kuwakamata kinaongeza soko.

Kwa upande wa Kenyela, alisema amesikitishwa na kauli za Kamanda Kiondo alizozitoa kwenye vyombo vya habari, ikiwa ni njia mojawapo ya kumdhalilisha.

Alisema Kamanda Kiondo, alikiuka taratibu za kijeshi kwa kumkosoa kiutendaji hadharani, badala ya kupeleka malalamiko kwa wakubwa wake au kumpigia simu na kushauriana kama anakwenda kinyume.

Mvutano huo, ulisababisha Kamanda Kova kuingilia kati na kuitisha kikao cha usuluhishi ambacho kilifanyika juzi usiku na kufanikiwa kuwapatanisha

No comments:

Post a Comment