Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wamefunga barabara kwa muda mkoani morogoro.
Waendesha pikipiki hao wamefunga barabaraya kutokea mjini
kuelekea kituo kukuu cha mabasi msavu eneo la masika wakipinga
utaratibu mbovu unaotumiwa na mamlaka ya kukusanya kodi mkoa wa morogoro
(TRA) Wa kuwakamata waendesha bodaboda hao bila utaratibu,Akisumulia
tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda hao amesema TRA
wameanza utaraibu wa kuwakimbiza waendesha pikipiki hao kwa kutumia
magari jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Akiendelea
amesema pia wamekuwa wakiwakamata kwa vurugu na bugudha kubwa bila
kujali wapo waliolipa kodi na ambao hawajalipa kodi.
Moto
uliowashwa na waendesha bodaboda hao waliofunga barabara mkoani morogoro
kwa kuchoma matairi, kupanga magogo,na mawe barabarani kwa lengo la
kuipinga uwonevu unaofanywa na mamlaka ya kukusanya mapatoya kukusanya mapato mkoa wa morogoro dhidi yao.Moto huo ukiendelea kuwaka kabla ya kudhibitiwa na jeshi la polisi mchana huu
Moto huo ukizimwa na kikosi cha zimamoto mkoa wa morogoro baada ya kufuka eneo la tukio
wakazi wa morogoro wakiwa wamesimama kando ya barabara hiyo kushuhudia tukio hilo mchana huu mjini morogoro
Mkuu wa kituo cha polisi morogoro mjini akiwa eneo la tukio kuhakikisha usalama na amani unakuwepo baada ya kufanikiwa kudhibiti tukio hilo
No comments:
Post a Comment