KLABU
ya Arsenal imetolewa katika Kombe la FA baada ya kufungwa na Blackburn
1-0 katika mchezo wa Raundi ya Tano Uwanja wa Emirates leo.
The
Gunners ambayo itapambana na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya Jumanne, leo iliwapumzisha wachezaji nyota kama Jack Wilshere,
Theo Walcott na Santi Cazorla ambao kocha Arsene Wenger aliwaanzishia benchi kabla ya kuwaingiza baadaye.
VIKOSI VYA LEO
Arsenal:
Szczesny, Vermaelen, Koscielny, Monreal, Diaby, Rosicky (Wilshere 70),
Arteta, Oxlade-Chamberlain (Cazorla 70), Coquelin, Giroud, Gervinho
(Walcott 70)
Benchi: Mannone, Sagna, Ramsey, Podolski
Kadi ya Njano: Coquelin
Blackburn:
Kean, Orr, Martin Olsson, Dann, G Hanley, Lowe, Pedersen, Marcus Olsson
(Bentley 63), Williamson, Rhodes (Goodwillie 83), Kazim-Richards
Benchi: Usai, Givet, Rekik, Nunes, Nuno Gomes
Kadi ya njano: Orr, Goodwillie
Mfungaji wa bao: Kazim-Richards dk72
Refa: Mike Dean
Mahudhurio: 60,070

Colin Kazim-Richards akiifungia Blackburn Rovers Uwanja wa Emirates


Gervinho akisikitika baada ya kukosa bao la wazi

Mikel Arteta akipiga mpira wa adhabu

Olivier Giroud (kulia) akikabiliana na mchezaji wa Blackburn, Jason Lowe (kushoto) kugombea mpira

Jack Wilshere (kushoto), Theo Walcott (katikati) na Santi Cazorla (kulia) wote waliingia kutokea benchi

Kipa wa Blackburn, Jake Kean leo alikuwa kikwazo kwa Arsenal

Alex Oxlade-Chamberlain (kulia) akijaribu kumtoka Grant Hanley (kushoto)

Tomas Rosicky alirejea kwenye safu ya kiungo ya The Gunners leo

Theo Walcott hoi

Kazim-Richards akishangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal

David Bentley (kulia) aliichezea kwa mara ya kwanza Blackburn iliyomchukua kwa mkopo dhidi ya klabu yake ya zamani

Refa Msaidizi, maarufu kama mshika kibendera, Sian Massey akikagua nyavu kabla ya mechi

No comments:
Post a Comment