Askofu Dkt Mdegela
Na .Said Ng'amilo Iringa.
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi
yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu
uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na
uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa
vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa
mpango huo.
Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa
ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi
hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati
huo.
Kufuatia hali hiyo, Mdegela amewaandikia waraka, wanachama wote
wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo nchini (CCT) kuanza mara moja
mfungo wa saa 24 kuanzia leo (Maombi ya mnyororo), kusali dhidi ya
uhalifu huo kwa minajili ya kuwasaidia makachero kutoka ndani na nje ya
nchikuwabaini wanaotekeleza mkakatihuo.
Dk. Mdegela alitoboa siri hiyo wakati akizungumza na Waaandishi wa
Habari katika kanisa kuu la kkkt lililopo eneo la Miyomboni sokoni
Manispaa ya Iringa.
No comments:
Post a Comment