Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, February 16, 2013

Beki Kapombe, ‘Messi’ kujaribiwa Sunderland


 
Simba wakifanya mazoezi, katikati ni mchezaji Kapombe 

WACHEZAJI wawili wa klabu ya Simba, Shomari Kapombe na Ramadhan “Messi” Singano wamekwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa na klabu inayoshiriki Ligi Kuu England, Sunderland.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Aden Rage alisema jana kuwa kuteuliwa kwa wachezaji hao kumetokana na viwango vyao na umri na endapo watafuzu, basi watacheza soka klabu hiyo ya England yenye historia kubwa nchini humo.
Rage alisema kuwa wameingia kwenye makubaliano maalumu na timu hiyo katika kuendeleza upande wa ufundi, uongozi na timu kwa jumla na hilo limetokana na historia ya Simba SC ambayo miaka ya 1960 ilikuwa inajulikana kwa jina hilo.
Alisema kuwa hatua hiyo ni faraja klabu ya Simba kutokana na ukweli kuwa matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa kama yalivyo kwa timu hiyo ya England.
Aliongeza kuwa wana mawasiliano mazuri na mmiliki na mwenyekiti wa timu hiyo, Ellis Short kuhusiana na mpango huo.
“Tumeweka mikakati mikubwa na kuhakikisha Simba inafikia hatua kubwa ya maendeleo. Tunaendelea na mazu ngumzo na viongozi wakuu wa timu hiyo na mwezi ujao, tuta kwenda huko kufanya mazu ngumzo zaidi na kukamilisha masuala mbalimbali,” alisema Rage.
Ujumbe huo utaongozwa na Rage na wengine watakaojulikana hapo baadaye. Safari hiyo itafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Machi.
Aidha, Rage alisema kuwa katika kuhakikisha ushirikiano wao unadumu, klabu hiyo itavaa jezi zenye nembo ya timu ya Sunderland kuanzia msimu ujao. Alisema kuwa ili kuondoa mtafaruku, jezi hiyo pia itakuwa na nembo ya wadhamini wao we ngine.
Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya klabu ya Simba, Rahma Al Haroos jana alikabidhi jezi mpya kwa klabu hiyo kwa ajili ya kutumika kesho katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya timu ya Recreative de Libolo ya Angola.
Alharoos alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi jezi hizo ni kuongeza morali kwa timu hiyo ili kushinda mechi hiyo.
Wakati huohuo Rage amesema kuwa fedha za ma lipo ya awali ya mchezaji wao, Emmanuel Okwi aliyeuzwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia hazijawafikia mpaka sasa. Etoile du Sahel ilimnunua Okwi kwa dola za kimarekani 300,000 (Shs 470 milioni).
Alisema kuwa timu hiyo ya Tunisia imeahidi kulipa kwa mikupuo miwili.

No comments:

Post a Comment