KINARA wa vurugu za kidini zinazoibuka kila siku ya Ijumaa jijini Dar es Salaam, amejulikana.
Kinara huyo ametajwa kuwa ni Sheikh Issa Kondo Bungo ambaye amekuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu bila mafanikio.
Habari
kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, zilisema
kuwa Sheikh Bungo anadaiwa kuhusika na matukio kadhaa makubwa ya vurugu
za kidini, zilizotokea kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam.
Duru za
kipolisi zilitaja baadhi ya matukio ambayo Sheikh Bungo anadaiwa
kuhusika nayo kuwa ni pamoja na tukio la kuchoma moto kanisa la TAG la
Mbagala, baada ya mtoto (jina limehifadhiwa), kukojolea Qur’an.
Tukio la
kukojolea kitabu hicho lilitokea Oktoba 10 katika eneo la Chamazi saa 10
jioni wakati watoto hao wakiwa katika ‘kijiwe’ chao cha kuchezea mpira.
Vurugu
hizo zilisababisha kuvunjwa kwa vioo vya magari, madirisha ya makanisa
pamoja na kuibwa kwa vifaa vya kwaya katika makanisa hayo ambayo ni ya
Anglikana, Wasabato na Pentekoste.
Kutokana
na tukio hilo ambalo liliibua vurugu kubwa kutoka kwa baadhi ya waumini
wa Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali, Sheikh Bungo anatajwa
kuhusika kushawishi wenzake kuchoma kanisa hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, Jeshi la Polisi limekuwa likimsaka kwa muda
mrefu, lakini halijafanikiwa kumtia mbaroni kutokana na staili yake ya
kuishi kwani hana makazi maalumu.
“Shekh
huyo pia anahusika kushawishi wafuasi wa Katibu wa Jumuia na Taasisi za
Kiislamu Ponda Issa Ponda kuandamana kila siku ya Ijumaa ili kushinikiza
mahakama itoe dhamana kwa Ponda ambaye kwa sasa yuko rumande
akikabiliwa na kesi ya uchochezi,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Kwa
mujibu wa habari hizo, tangu tukio la vurugu za Mbagala lilipotokea,
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata wafuasi wa sheikh huyo na
wengine wako mahakamani, lakini yeye hajapatikana.
Tayari Sheikh Bungo pamoja na wenzake wamefunguliwa kesi namba THA/ IR/ 7794/ 2012 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
No comments:
Post a Comment