Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali.
Alisema
kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa jeshi hilo Padri Mushi
,alipigwa risasi akiwa kwenye ndani ya gari na kujeruhiwa vibaya sehemu
za kichwa na kifua.
Alisema
baada ya kutokea kwa tukio hilo punde baadhi ya waumini wa kanisa hilo
waliofika katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada walimpeleka Padri Mushi
katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu baada ya muda
mchache Akafariki dunia.
Kutokana
na uzito wa tukio hili jeshi la polisi Zanzibar linaendelea na
upelelezi wa kina kuhakikisha wahusika wote wanafikishwa katika vyombo
vya kisheria.”Alisema kamishna Mussa
Hii ni gari aliyokuwamo Padri Mushi.
Natoa
wito kwa wananchi washirikiane na maafisa wetu juu ya taarifa zozote
zinazohusiana na tukio hili ili tuweze kutekeleza majukumu kwa wakati.”
Aliendelea kusisitiza
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ,ACP Aziz Mohamed alisema
kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na doria katika maeneo mbalimbali
ya Mjini wa Zanzibar ili kuhakikisha wale wote wanaohusika katika mauaji
ya padri huyo wanakamatwa.
Wakati
huo huo ,Naye Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Abdallah Mwinyi Amefika
katika Viunga vya Hospitali ya Mnazi Mmoja Mnamo wa Saa 4 Asubuhi kwa
ajili ya kuwafariji Jamaa,ndugu na waumini wa dini hiyo waliofika katika
eneo hilo kwa ajili ya kufuatilia hatima ya kiongozi wao.
Akizungumzia
tukio hilo,msemaji wa kanisa hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa
katoliki,jimbo la Zanzibar padri Cosmas Shayo aliwataka waumini wa
kanisa hilo,kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki hadi suala hilo
litakapotafutiwa ufumbuzi.
Alisema
Uongozi wa kanisa hilo,umepokea suala hilo kwa masikitiko makubwa pia
kufariki kwa padri huyo ni miongoni mwa pigo kubwa kwa waumini na kanisa
kwa ujumla.
Tukio
hili si la kufumbia macho kwani viongozi na waumini wa kanisa katoliki
Zanzibar kwasasa tunaishi kwa mashaka hali ya kuwa,mtu ukitoka asubuhi
huna uhakika wa kurudi jioni ukiwa hai”Alisema padri Shayo.
Kwa
nini matukio haya yanaandama waumini na viongozi wa kanisa katoliki
hapa kuna agenda ya siri hadi tunafikia hatua ya kuishi kama watumwa
tukiwa na hofu juu ya usalama wa maisha yetu,serikali na vyombo vya
ulinzi vikiwa vinakaa kimya.”Aliendelea kusema Padri shayo.
Alisema
Kanisa linathamini mchango mkubwa uliotolewa na marehemu wakati wa uhai
wake,katika kuliendeleza kanisa kwenye huduma za kiimani na kiroho kwa
waumini wa kanisa.
Baadhi
ya mashuhuda ,waliozungumza kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio
ambapo walisema kwamba walifika mapema katika Kanisa hilo kwa ajili ya
maandalizi ya ibada,pembeni mwa kanisa hilo kulikuwa na watu watatu
ambao hawakujulikana kwa haraka ghafla baada ya kufika padri Mushi
walisikia milio ya risasi wawili wakaondoka mbio na pikipiki aina ya
vespa na mmoja akatokomea Vichochoroni.
Padre
Evaristus Mushi ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao
walikua wamepanda pikipiki aina ya Vespa leo asubuhi wakati akielekea
kuongoza misa katika kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.
Wananchi
wamesikika wakitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti
uharifu na umiliki wa silaha kinyume cha sheria,kwani matukio ya
kushambuliwa kwa viongozi wa dini mbalimbali Zanzibar yameshamili.Wakati
huo huo ,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi amesema
serikali itahakikisha inafanya juhudi kuhakikisha inawakamata watu
waliomuua Padre Evarist Mushi wa kanisa katoliki Zanzibar.Akizungumza
na waandishi wa habari huko Makao makuu ya Polisi Zanzibar Dkt, Nchimbi
amesema serikali imesikitishwa na tukio hilo alilolieleza kuwa ni la
kigaidi huku akishtumu kuwa wana lengo la kuingiza nchi katika
machafuko.
Amesema kuwa tukio hilo si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika kuwashambulia viongozi kidini.
Amesema
kuwa tukio hili limefanana na tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana
la kushambuliwa kwa risasi Padre Ambrose Mkenda wa Kanisa katoliki
parokia ya Mpendae
Amesema
kuwa katika kukabiliana na matukio ya kihalifu hapa nchini Wizara
imeomba kibali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikia na
mashirika ya kimataifa ya upelelezi ili kuwakamata wahalifu hao.
Dkt,
Nchimbi amewataka Watanzania kuwa wavumilivu na kujiepusha katika mtego
wa kuchukia na kwa misingi ya kidini katika kipindi hichi ambacho
Jeshila Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment