Mmoja wa
mapadre waandamizi wa kanisa katoliki nchini Uingereza amejiuzulu
wadhifa wake kufuatia shutma za kwamba alikwenda kinyume na matakwa ya
kipadre mapema miaka ya themanini.
Kardinal Keith O'Brien ameachia madaraka
kama kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Scotland na hatarajii
kusafiri kwenda Vatican baadaye mwaka huu kumchagua Papa ajaye baada ya
baba Mtakatifu Benedict wa 16 kijuzuru.
BBC imeelezwa kuwa kiongozi
huyo,ameshutumiwa na mapadre watatu wa kanisa hilo na hatua hiyo ya
kujiuzulu ni tukio kubwa katika mwenendo wa kanisa katoliki ikizingatiwa
kuwa Kanisa hilo limekuwa kwenye shutma za ulaji rushwa na matatizo ya
kiongozi kwa siku za hivi karibuni.
Inaarifiwa Padre O'Brien aliwauvinjia heshima makasisi mingo mitatu iliyopita.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, alisema kuwa anapinga vikali madai hayo.
Duru zinasema kuwa hatua ya kujizulu kwa
padre huyo kunaongeza shinikizo kwa makadinali wengine wanaokabiliwa na
tuhuma za walivyoshughulikia kashfa za ngono
No comments:
Post a Comment