Mwili wa mtu huyu ulikutwa umetupwa maeneo ya Tegeta-Kondo ndani ya uzio wa kiwanja karibu na makaburi ya Kondo juzi tarehe 21-02-2013 sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa kama anavyoonekana.
Polisi walikuwepo wakiwahoji wakazi wa nyumba iliyo ndani ya uzio huo.
Nimeongea sasa hivi na mtu wa maeneo hayo kujua kilichojiri, ni kwamba huyo mtu alikuja kutambuliwa, ni mzee aliyekuwa mlinzi kwenye baa ya mzee mmoja anaitwa Mwaipopo iko maeneo ya Bahari Beach, baada ya kutoonekana kazini watoto wa huyo mzee katika kufuatilia ndo wakaja kugundua ndiye aliyekuwa amekufa pale (walimtambua baada ya kufukuliwa) ingawa ilibidi azikwe maeneo hayohayo kutokana na mwili wake kuwa umeharibika sana.
NKASI YAJENGEWA UWEZO MASUALA YA MENEJIMENTI YA MAAFA
-
NA. MWANDISHI WETU -NKASI
Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na
Wenye Ulemavu imewajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya...
11 minutes ago



No comments:
Post a Comment