Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, February 23, 2013

SERIKALI YA DK KIKWETE YAONGOZA KWA KUKOPA, DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILIONI 21.



YAKOPA MARA MBILI ZAIDI YA ZILIVYOKOPA AWAMU YA TATU ZILIZOPITARais wa awamu ya nne Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na vyombo vya habari siku za hivi karibuni 

TAASISI isiyo ya kiserikali ina yojishughulisha na masuala ya Madeni ya Taifa na Maendeleo (TCDD), imesema Serikali ya Tanzania ndiyo inaongoza kwa kukopa zaidi, ikieleza kuwa kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2011, imekopa kiasi cha Sh15trilioni na kufanya deni la taifa kufikia Sh21trilioni.
Rais Kikwete aliingia madarakani mwaka 2005, baada ya rais aliye mtangulia, Benjamin Mkapa kumaliza kipindi chake cha uongozi wa miaka 10 kilichoanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005.
TCDD imebainisha kuwa Serikali inakopa fedha hizo kutoka Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii. Pia inakopa katika taasisi za kimataifa ikiwamo, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF).
Katika maelezo yake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Hebron Mwakagenda, alisema kuwa kite ndo cha Serikali kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yasiyo muhimu pamoja na kuwalipa watumishi wake mishahara, ndiyo sababu ya kukua kwa deni hilo la taifa.
“Serikali ya awamu ya nne imekopa kwa kiwango kikubwa, kwani tangu iingie madarakani imeshakopa Sh15trilioni, sasa sijui mpaka inamaliza muda wake itakuwa imekopa kiasi gani?” alisema Mwakagenda akihoji na kuongeza;

No comments:

Post a Comment