Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 21, 2013

SIRI YA KUFELI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE 2012 YAFICHUKA.



MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI, KABWE ZITTO.

MITIHANI kusahau wenye welewa wa kawaida na wa chini, ndiyo siri kubwa ya kufeli kwa watahiniwa wa kidato cha nne katika matokeo yaliyotangazwa juzi Dar es Salaam, imeelezwa.
Hali hiyo ilitokana na maswali yaliyotolewa kuwa ya kitaalamu zaidi na hivyo kuwa magumu kwa wanafunzi wengi kiasi cha kushangaza hata shule zilizokuwa zikifanya vizuri zamani.
Akitoa maoni juu ya wanafunzi wengi wa kidato cha nne kufeli, Mwalimu wa Taaluma wa kundi la shule za Feza, alisema matokeo hayo yameishangaza shule hiyo na hivyo kukosa mwanafunzi mwenye ushindi wa alama saba kama ilivyozoeleka.
Mwalimu Simon Albert alisema jana, kwamba “maswali yalikuwa ya kitaalamu zaidi,” na kutoa mfano kwamba mbali na masomo ya Hisabati na Biolojia, masomo mengine yalikuwa magumu kwa kiwango cha wanafunzi wengi.

No comments:

Post a Comment