Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 7, 2013

TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA 2013 ZAZINDULIWA RASMI



Pichani katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za wanawake wenye Mafanikio Tanzania bi. Sadaka Gandi akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na mchakato mzima wa tuzo hizo, kulia Raisi wa tuzo hizo bi. Irene Kiwia na kushoto ni bi. Esther Shayo mratibu.

Pichani kulia ni Raisi wa tuzo hizo Irene Kiwia akielezea jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na tuzo hizo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013, zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.

Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.

"TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa si tu kibinafsi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na  michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufariji na kuridhisha sana.”

Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi naTeknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.

Bi SadakaGandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteuawa na wake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili watuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wamabadiliko katika jamii zao.

Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "

Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu yaMtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello – Kamishna waTume ya Hakiza Binadamu naUtawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga-Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi.Ludovicka Tarimo–Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlakaya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.

Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwana Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, WatuwaMarekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.

No comments:

Post a Comment