Polisi
nchini Kenya wanasema wamepata vijikaratasi vya uchochezi dhidi ya
makabila tofauti katika baadhi ya sehemu nchini humo, siku chache tuu
kabla ya uchaguzi mkuu. Vijikaratasi vya uchochezi vilitumika pakubwa wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata wa mwaka wa 2007.
Pia vingine vilipatikana mjini Mombasa ambako kundi linalotaka kujitenga kutoka Kenya, mkoani Pwani, lina makao yake.
Mjini Kisumu, Polisi ilisema vijikaratasi hivyo vilikuwa vikichochea wakaazi dhidi ya watu kutoka jamii tofauti.
Kimaiyo anasema uchunguzi unaendelea lakini hakuna mshukiwa yoyete aliyekamatwa hadi kufikia sasa.
No comments:
Post a Comment