Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 22, 2013

WAKAZI WAANDAMANA KUZUIA MITI KUKATWA MOROGORO

 





Wakazi wa madizini kata ya boma mkoa wa morogoro wameandmana kupinga miti iliyo katika mtaa wao kukatwa kwa kuwa hawakushirikishwa na viongozi wa mtaa wao.wakazi hao wengi wakiwa vijana walindaman leo asubuhi kwa kuzunguka maeneo yote ambayo miti tayari imeshakatwa kwa lengo la kusimamisha zoezi hilo kwa kuwa halikufuata utaratibu.
Wakazi hao pia wamelalamikia vibali vivivyotumika kutokuwa halali,Vijana hao wakizungumza asubuhi ya leo wamemuomba mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera kuingilia Mgogoro huo kwa lengo la kunusuru maliasili hiyo ambayo inatoweka kwa kasi mtaa wa madizini kata ya boma mkoani morogoro.
Wakazio hao wanapingana na viongozi wao akiwepo diwani ya kata hiyo Mh Amir Nondo na mwenyekiti wa mtaa aliyefahamika kwa jina moja la Mashaka.


Waandishi wa habari wakiwa eneo hilo kujua meni zaidi kutoka mtaa huokuhusu mgogoro huo
Miti  iliyovunwa ambayo inalalamikiwa na wakazi wa mtaa madizini kata ya boma mkoani morogoro.

Moja ya vibali walivyokuwa navyo wakazi hao




Kibali kilichotolewa kwa ajili ya ukataji wa miti hiyo jambo linalolalamikiwa kuwa nifeki kwa kuwa hakina muhuri wowote.
Mkazi wa mtaa huo wa madizini aliyefahamika kwa jina moja la Eric akihojiwa leo eneo la tukio kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo walipoenda kuonyesha miti ilyokwisha katwa na mfanya biashara mmoja kutoka tanga..audifacejackson blog
Baadhi ya wakazi hao waliokuwa katika sekeseke hilo leo asubuhi.
Wakazi hao wakiwa eneo la tukio leo hapa wakiimba' hatutaki miti yetu hii ndiyo gesi yetu;
audifacejackson blog
wakiimba na kushangilia mara baada ya kufanikwa kusimamisha zoezi hilo


mashuhuda wa tukio hilo leo

Miti aina ya mitiki iliyovunwa na kuleta kizaa zaa

No comments:

Post a Comment