Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 18, 2013

WAZIRI MKUU PINDA ASUSIWA KATIKA KIKAO NA VIONGOZI WA WAISLAM JUU YA SAKATA LA UCHINJAJI WANYAMA WA KITOWEO MKOANI GEITA.



WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA. 
VIONGOZI wa dini ya Kiislamu mkoani Geita wamesusia kikao cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusuluhisha mgogoro wa uchinjaji baina yao na viongozi wa dini ya Kikristo.
Viongozi hao wametoa masharti ya kuachiwa wenzao sita waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Buseresere, Mathayo Kachila (45).

Kikao hicho ambacho kilidumu kwa muda wa dakika 45,  kilivunjika baada ya viongozi wa Waislamu kutaka kuachiwa kwa wafuasi wao baada ya wafuasi wa dini ya Kikristo kuachiwa baada ya vurugu zile.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada viongozi hao kuondoka,
Pinda alisema kikao chake kimeshindikana kutokana na viongozi wa dini ya Kiislamu kutoa masharti ambayo yapo nje ya uwezo wake.

No comments:

Post a Comment