Arusha.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini,
kimetangaza mgogoro na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo na
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Gilles Bilabaye .
Hatua hiyo inatokana na kile kinachodai
walitumia lugha na kauli za matusi dhidi ya wanachama na wafuasi wa
chama hicho, kwenye harakati za kuzuia maandamano yaliyoitishwa
kumshinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa
ajiuzulu.
Akisoma tamko la chama hicho kwa
waandishi wa habari jana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema
viongozi hao waliwaita vijana wafuasi wa Chadema kuwa ni wahuni, wavuta
bangi na wanywa viroba.
Pia, wanadaiwa kuwaita wafuasi hao kuwa
hawana kazi za maana, ndiyo maana wanakubali kushiriki maandamano
yanayoitishwa na chama hicho.
“Tunatoa muda wa siku tatu kwa viongozi
hao kutumia njia ileile ya redio za masafa mafupi Arusha na magari ya
matangazo walizotumia kutoa matusi hayo, kuomba radhi kwa vijana wa
Arusha,” ilisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Kanda hiyo,
Amani Golugwa.
No comments:
Post a Comment