MWANAMUZIKI
Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni aliwachefua waumini wenzake wa
dini ya Kiislam baada ya kutinga kwenye Maulidi akiwa amevaa hereni na
cheni.
Tukio
hilo lilijiri maeneo ya Tandale, Dar ambapo mama yake aliyemtambulisha
kwa jina la Aunt Shani aliandaa maulidi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi
Mungu.
Akiwa
mmoja wa waalikwa, Diamond alinaswa akiomba dua sambamba na rafiki yake
aitwaye Remeo Jones ‘RJ’ huku akiwa amevaa kanzu safi na balaghashia
lakini akaharibu kwa kuvaa hereni na cheni.
Kitendo
hicho kiliwachefua Waislam ambapo baadhi walifikia hatua ya kumchana
laivu kuwa, alichokifanya kilikuwa kinyume na Uislam.
No comments:
Post a Comment