Lema aitisha maandamano
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,
Godbless Lema, ametangaza kuandaa maandamano makubwa yatakayoshirikisha
wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili kushinikiza Mamlaka ya
Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) kuwasambazia maji.
Akizungumza jana, Lema alisema
ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi ya miezi
sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji safi.
“Nimewaandikia
barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi
na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge
ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa
tutawashinikiza kwa nguvu wa umma,” alisema Lema.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa AUWSA, Mhandisi Ruth Koya hakupatikana
kuelezea kama amepokea barua hiyo baada ya kutopatikana ofisini, pia
simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.
No comments:
Post a Comment