Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
JINA la Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimaitafa, Bernard Membe, limeanza kuhusishwa na
tukio la kutekwa na kuteswa kikatili na watu wasiojulikana lililomkuta
Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda.
Madai ya kulihusisha jina la
Waziri Membe na tukio hilo, yalianza kuzagaa miongoni mwa watu waliofika
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Kibanda, muda
mfupi baada ya kutendewa unyama huo.
Makundi ya watu waliokuwa
hospitalini hapo walilioanisha tukio hilo na kauli iliyopata kutolewa na
Waziri Membe katika mahojiano ya kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa
na Kituo cha Televisheni cha ITV, alipoeleza kuwa anao maadui wakubwa
11, wakiwamo waandishi wa habari wawili ambao aliahidi kuwashughulikia.
Ingawa Membe alikutana na
shinikizo la watu mbalimbali lililomtaka awataje maadui zake hao 11,
wakiwamo waandishi wa habari wawili ambao alikuwa na mpango wa
kuwashughulikia, hadi sasa hajapata kufanya hivyo, jambo ambalo
linadaiwa na wadadisi wa mambo kuwa ni uamuzi wake wa kuchukua mkondo wa
kutekeleza kile alichokisema kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment