Zacharia Hans Poppe; Amejiuzulu Simba SC |
Na Mahmoud Zubeiry
, amejiuzulu wadhifa wa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC ya dar
es Salaam pamoja na Uenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo leo.
Kwa mujibu wa habarikutoka ndani ya Simba mida hii, Hans Poppe
amewasilisha barua ya kujiuzulu leo akielezea kusitikishwa kwake na hali
halisi ndani ya klabu.
Alipoulizwa mwenyewe kuhusu hilo, alisema; “Sipo katika nafasi ya
kulizungumzia hilo kwa sasa, wasiliana na Katibu (Evodius Mtawala) au
Mwenyekiti (Alhaj Ismail Aden Rage),” alisema Hans Poppe, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Friends of Simba na kukata simu.
Mtawala na Rage hawakupatikana kwenye simu zao mida hii, ingawa BIN ZUBEIRY inaendelea na juhudi za kuwatafuta.
Kwa mujibu wa barua hiyo, pamoja na kujiuzulu, Hans Poppe ameahidi kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu ndani ya Simba SC.
Wazi kujiuzulu kwa Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) ni pigo kwa klabu hiyo, kwani alikuwa akiisaidia mno kwa hali na
mali.
Aidha, kujiuzulu kwa Hans Poppe wazi kutachochea zaidi mgogoro ndani ya
klabu hiyo na kuongeza shinikizo la viongozi wa klabu hiyo kujiuzulu
pia.
Simba SC kwa sasa haifanyi vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara na tayari imekwishatolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya
kufungwa jumla ya mabao 5-0 na Recreativo de Libolo ya Angola katika
raundi ya kwanza tu.
Ubingwa wa Ligi Kuu ni kama
umekwishaota mbawa, kwani hadi sasa Wekundu hao wa Msimbazi wanashika
nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31, sawa na Coastal Union ya Tanga na
Mtibwa Sugar ya Morogoro, nyuma ya Azam FC yenye pointi 36 na Yanga
inayoongoza kwa pointi zake 42, zote za Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment