Kikosi cha Jeshi kikiwasili eneo la tukio kusaidia shughuli ya uokoaji.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa
Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
Juhudi zinaelekea kulala.........
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Trekta likiendelea kuondosha kifusi.
Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.
Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na
zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.
Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi
wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho
kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo
hayo.
Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.
No comments:
Post a Comment