Na Dustan Shekidele, Morogoro
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina
la Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu
ya aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akingonoka’ na shemeji yake.
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu
mchana kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha
Mbaji Hamis ambaye ni mdogo wa Mrisho.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Mrisho ambaye anafanya kazi ya kupiga debe katika
stendi ya mabasi ya Msamvu alisema, fumanizi hilo halikutokea kwa kuweka
mtego bali ni Mungu tu.
Alieleza
kuwa alikamatwa Ijumaa na kutupwa mahabusu kwa kosa la kutovaa
‘yunifomu’. Mkewe na mdogo wake wakawa wanampelekea chakula.
No comments:
Post a Comment