WAKATI
wananchi wengi, wakikabiliwa na ugumu wa maisha, madereva wa wabunge
nao wameibua kilio chao wakilalamikia ukali wa maisha. Madereva hao,
walilazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila
wakilalamikia haki zao kukaliwa na wabunge. MTANZANIA imefanikiwa kunasa
barua hiyo ya Julai, 2012 ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa
Madereva wa Wabunge, Juvenille Joseph.
Pamoja na
mambo mengine, barua hiyo inaishutumu Ofisi ya Bunge kushindwa
kusimamia maslahi yao, hali inayowafanya waishi kwa shida.
Katika
barua hiyo, madereva hao walilamikia suala la ukosefu wa mikataba ya
kazi, huku wakitaka posho na mishahara yao itenganishwe kutoka katika
akaunti za wabunge.
“Mheshimiwa
Katibu wa Bunge, sisi ni madereva wa waheshimiwa wabunge, tunaleta
kwako hoja zetu ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kina katika ofisi yako.
“Kwa kipindi chote, madereva wa wabunge hatukuwa na mikataba ya ajira zaidi ya makubaliano ya mdomo baina ya dereva na mbunge.
“Ndiyo maana kunakuwa na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge dhidi ya madereva wao.
No comments:
Post a Comment