Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi
katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli
za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu
waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni
17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Uokoaji ukiendelea.....
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16,
lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki.
Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea,
ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia
watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Askari
Jeshi wakikokota Jenereta kubwa kusogeza eneo la tukio ili kuhakikisha
mwanga unapatikana kurahisisha shughuli za uokoaji hadi usiku, baada ya
giza kuingia.
No comments:
Post a Comment