Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha
kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa na jeraha lolote.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na
Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu
alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwa mwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba
funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala
na wanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili
ya masomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla
hajajiunga na chuo hiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea
mara kwa mara,” alisema Mushi.
No comments:
Post a Comment