Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu,
Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili
wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani
Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka
kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga
mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba,
Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili
Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika
kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani
CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa
katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi.
Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa
Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa
Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim
Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba
kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili
Waombolezaji
wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF,
aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye
gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa
maziko, yatakayofanyika leo. Picha na OMR
Wanafamilia ya Marehemu, Salim Hemedi Khamisi, Mbunge wa Chambani wakilia kwa uchungu Salim Hemedi Khamisi
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Wananchi CUF wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakijadili
jambo wakati wakisubili mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamisi, Mbunge wa Chambani Pemba, Dar es Salaam. Baadhi
ya familia ya Mbunge wa Chambani Marehemu, Salim Hemedi Khamisi, wakiwa
na hudhuni kumwa baada ya mpendwa wao kufaliki dunia.
Mke
wa Mbunge wa Chambani Marehemu Salim Hemedi Khamisi wa pili kulia, Asla
Saidi Zaharani, akilia kwa uchungu baada ya kupewa taalifa ya kifo cha
mume wake.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda, akiwafaliji viongozi wa Chama cha wananchi CUF
kutokana na kifo cha mbunge wao,Salim Hemedi Khamisi,Salim Hemedi
Khamisi, katika Hosptali ya Taifa Muhimbili
Spika wa Bunge, Anne Makinda,akimfariji Mke wa Marehemu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto wa Marehemu, Salim Hemedi Khamisi wakiwa na hudhuni kutokana na kifo cha baba yao mpendwa.
Spika wa Bunge akiwafariji wanandugu wa marehemu Mbunge wa Chambani, Salim Hemedi Khamis
Waziri wa Ulinzi, Shamshi Vuai Nahodha,akisalimiana na wanafamilia wa marehamu, Salim Hemedi Khamis
Mwili
wa Marehemu ukungizwa katika Gari kwaajili ya kuupeleka katika msikiti
wa Shadhiri kwa jili ya kuhifadhiwa.Picha Kwa Hisani ya Habari Mseto
Blog
No comments:
Post a Comment