Mwenyekiti
wa Taasisi ya Figo Tanzania Mh. Frederick Werema akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kunywa
maji safi na salama kama moja ya njia za kukinga figo kuathiriwa na
magonjwa mbalimbali na kutoa wito kwa watanzania kuepuka tabia hatarishi
kwa afya ya figo zikiwemo za utumiaji wa pombe kupita kiasi, madawa ya
kulevya, utumiaji wa dawa za binadamu kupita kiasi na uvutaji
wa sigara. Picha na Aron – MAELEZO.
…………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
Watanzania
wametakiwa kujenga tabia ya kuvitumia vituo vya afya kupima afya ya
figo mara kwa mara na kupata ushauri na tiba mapema pindi
wanapogundulika kuwa na matatatizo ya figo ili kuepuka kusababisha
usugu wa ugonjwa huo.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi ametoa kauli hiyo leo
jijini wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya Siku ya Afya duniani
yatakayofanyika tarehe 14 mwezi huu duniani kote.
No comments:
Post a Comment