Mrisho
ngasa wa timu ya Simba akijaribu kumtoka beki wa Libolo ya Angola katika
mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam.
SIMBA leo
wanakabiliwa na mtihani wa kufanya maajabu mengine katika historia ya
soka Tanzania wakati watakapowavaa Recreativo Libolo ya Angola ugenini,
huku Azam FC wakishuka dimbani kulinda ushindi wao wa mabao 3-1
waliopata dhidi ya Al Nasri ya Sudan Kusini.
Pambano la Azam linafanyika kwenye mji wa Juba, ambapo wanahitahi sare aina yoyote ili kusonga mbele raundi ya pili
Katika
pambano la Simbalitakalochezwa saa tisa za Angola ikiwa ni saa 11 kwa
saa za Afrika Mashariki na kati, Simba wataingia katika uwanja wa
Calulukuumana na Libolo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 wiki
mbili zilizopita muuaji akiwa Joao Martins.
Katika
pambano la leo, kocha Patrick Liewing huenda akamkosa kiungo mahiri,
Mwinyi Kazimoto ambaye tangu awasili nchini Angola amekuwa akisumbuliwa
na jino.
Nafasi
yake inatazamiwa kuchezwa na kinda, Abdallaa Seseme ambaye alikuwa nyota
wa mchezo katika pambano la Ligi kuu dhidi ya Prisons wiki moja
iliyopita. Kama Kazimoto akipata nafuu kabla ya mechi basi huenda Seseme
akaanzia benchi.
Kocha
Liewig ambaye ni raia wa Ufaransa amepanga kucheza soka la kushambulia
na kutengeneza nafasi kwa ajili ya kurudisha bao la Martins ambalo
limeiweka Simba katika nafasi mbaya ya kusonga mbele.
Tutajaribu kufunga mabao ya mapema kwa ajili ya kurudisha bao lao.
Najua
wachezaji wangu wanaweza kufanya hivyo kwa sababu katika mechi ya kwanza
tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukutumia, wao walitengeneza
chache na walitumia,î alisema Liewing.
Liewig
pia aliongeza kuwa kutokana na wachezaji wengi wa Libolo kuwa na nguvu,
stamina atawataka wachezaji wake wajaribu kukaa na mpira kwa muda mwingi
wakiepuka matumizi ya nguvu ya Libolo.
Pambano
hilo linatazamiwa kuchezeshwa na Mwamuzi wa kati, Nhleko Simanga kutoka
Swaziland , waamuzi wasaidizi ni Nkhabela Bhekisizwe na Mbingo Petros
pamoja na mwamuzi msaidizi Fabuze Mbongiseni wote kutoka kutoka
Swaziland pia. Kamisaa wa pambano hilo ni Mandla Mazibuko kutoka Afrika
Kusini.
Mwamuzi
Simanga anaweza kuwa na bahati nyingine kwa Simba leo kwa sababu ndiye
aliyechezesha mechi kati ya Simba na Shandy ya Sudan, ambapo Simba
walishinda 3-0 kwa mabao ya Emmanuel Okwi, Haruna Moshi na Patrick
Mutesa Mafisango ambaye kwa sasa ni marehemu.
Endapo
Simba itashinda leo itakuwa imerudia historia ya mwaka 1979 ambapo
ilifungwa 4-0 nyumbani na Mufulira Wanderers, lakini ikashinda 5-0
ugenini jijini Lusaka.
Katika
pambano la leo, Simba ambayo imefikia katika Hotel ya Ritz inayomilikiwa
na tajiri wa Libolo, Lui Compos inatazamiwa kuwakilishwa na Juma
Kaseja, Said Nassor Chollo, Amir Maftah, Juma Nyosso, Komanbil Keita,
Shomari Kapombe, Haruna Chanongo, Amri Kiemba, Abdala Seseme, Felix
Sunzu, Mrisho Ngassa.
No comments:
Post a Comment