Gari la wema likiondoka maeneo ya ajli hiyo
Wema
Sepetu amepata ajali mbaya baada ya gari ambalo alikuwa akiliendesha
aina ya Audi Q7 kuacha njia na kugonga gari lingine kisha kumgonga
mtembea kwa miguu.
Tukio
hilo ambalo lilivuta umati wa watu lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa Wema
alikuwa katika mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo
barabarani.
Ajali hiyo ilisababisha foleni na baadhi ya vijana wanaosadikiwa ni vibaka kuanza kumzingira.
Kwa
mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na
mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi,
hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.
“Yaani mi nahisi alikuwa na mawazo mengi au alikuwa ‘amepata’ kidogo,” alisema shuhuda huyo aliyedai aliona mchezo mzima.
Baada ya kugonga, ilidaiwa kuwa mwigizaji huyo alishuka kwenye gari na kutaka kumpiga
vibao mtembea kwa miguu huyo lakini ghafla watu waliingilia kati na
kumzuia huku wakimuonya kuwa akithubutu wangemshushia kichapo.
“Huyu dada vipi? Ajali amesababisha yeye halafu anataka kumpiga mtembea
kwa miguu, angejaribu tu tungemvua nguo hapahapa,” alisema shuhuda mmoja
aliyekataa kuchorwa jina lake gazetini.
Paparazi wetu alipotonywa na kufika eneo la tukio, alilishuhudia gari
la mwigizaji huyo likiwa limebondeka kwa mbele huku akiliendesha
kulipeleka katika gereji iliyokuwa karibu na eneo hilo.
Hata hivyo, Wema alipomuona paparazi akiwa na vitendea kazi vyake
akimfuatilia kwenye gereji hiyo, aliondoa gari lake haraka ambapo umati
uliokuwa ukifuatilia kwa makini tukio hilo ulimzomea. Haikufahamika
alilipeleka wapi.
credit-globalpublishers
No comments:
Post a Comment