Chama
cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) kimesema kinaiburuza kortini
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra), kwa
madai kuwa hakikushirikishwa kwenye mchakato wa kuongeza nauli za
abiria.
Aidha, Chakua kimeitaka serikali kuuwajibisha uongozi wa juu wa Sumatra kwa kuifuta na kuunda upya kwa madai kwamba imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mshauri wa chama
hicho, Wilson Mashaka, alisema tangazo la kupandisha nauli halikujengwa
kwa dhana ya ushirikishwaji, kwani vikao vilivyofanyika kati ya Septemba
na Novemba, 2012, vilifanyika kwa kuwashirikisha wamiliki wa mabasi
lakini wadau muhimu kama Chakua hawakushirikishwa.
No comments:
Post a Comment