Msukule.
Na Makongoro Oging', Bagamoyo
INATISHA na
hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa
hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini
kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni
kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na
kuchukuliwa kimazingara.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Habari kutoka kijijini hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya shilingi 200,000 hadi 250,000 kwa kila mtu.

No comments:
Post a Comment