Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji
Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3,
huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika
leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya
shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
kesho.
Mmoja
wa majaji akibeba picha ya marehemu wakati majaji hao wakishuha jeneza
hilo lenye mwili wa marehemu, ili kuanza shughuli za kuaga katika
viwanja vya Karimjee leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwafariji ndugu wa marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho, wakati
wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest
Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.
Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo kwenye Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili
ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho.
Mmoja wa wanafamilia akibugujikwa machozi wakati wa shughuli hiyo ya kuaga.
Majaji
wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest
Mwipopo, wakishusha katika gari kwa ajili ya kuanza shughuli za kuaga
katika viwanja vya Karimjee, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakati akiwasili kwenye
Viwanja vya Karimjee leo kushiriki kwenye shughuli za kuaga mwili wa
marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya
gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Jaji Mkuu
Kiongozi na Jaji Mkuu wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga mwili.
SOURCE LUKAZA
No comments:
Post a Comment