Ludovick Utouh. |
Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ameshauri
kampuni za simu zinazotoa huduma ya utumaji fedha na kumbi za harusi
vitozwe kodi.
Sambamba na hilo aliutaka uongozi wa Bunge, kurejesha Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa
habari baada ya kuwasilisha taarifa yake bungeni mjini hapa jana akisema
uamuzi wa kufuta kamati hiyo na kazi zake kuunganishwa na Kamati ya
Hesabu za Serikali (PAC), hautakidhi matarajio ya wadau wa uwajibikaji.
Kwa upande wa kodi, alishauri kodi kutoka
kwa wafanyabiashara wadogo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ihusishe
kikamilifu makatibu kata kutambua walipa kodi wakiwamo wamiliki wa kumbi
za harusi na mikutano.
No comments:
Post a Comment