KUSHOTO: Padri William akimbusu mkewe, Beverley. KULIA: Kanisa la Mt. Clara ambamo Padri huyo alibambwa akifanya uchavu wake kwa binti wa miaka 17. |
Padri
mmoja wa kanisa Katoliki ambaye alifunga ndoa kwa siri amehukumiwa
kifungo cha miezi sita jela jana kwa kumsumbua msichana mdogo kwa kile
jaji alichoelezea 'uvunjifu mkubwa wa uaminifu'.
William Finnegan, akifahamika kama 'Fadha
Bill', alimpapasa binti huyo mwenye miaka 17 chini na kulazimisha
kumbusu kwa nguvu katika Kanisa Katoliki la Mt Clara mjini Bradford siku
ya Jumapili ya Pasaka mwaka jana.
Jaji Roger Thomas alisema kwamba Padri huyo
mwenye miaka 60, alikiri wakati wa kesi hiyo kwamba alifunga ndoa kwa
siri miaka 14 iliyopita.
No comments:
Post a Comment