Mahmoud Ahmad Arusha
Mtu
mmoja amefariki dunia baada ya kuvamiwa na majambazi na kupigwa risasi
ya shingoni wakati akiendesha gari kwenye maeneo ya barabara ya
Makongoro karibu na ofisi za Auwsa jijini hapa na watu watatu ambao ni
wanawake wawili na askari wa kikosi cha usalama barabarani kujeruhiwa
katika tukio hilo ambapo hadi sasa hawajatambuliwa majina.
Tukio
hilo limetokea leo majira ya saa 6:30 mchana maeneo hayo wakati
majambazi hao waliokuwa kwenye usafiri wa pikipiki kulivamia gari hilo
na kupora kiasi kikubwa cha fedha majira ya saa 5 na nusu mchana na
kukimbia kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment