Matuzya alisema jijini Dar es Salaam kuwa kiungo huyo alifanya mazoezi asubuhi na wenzake, lakini baadaye alimtaka kwenda kujiandaa kwa ajili ya upasuaji huo mdogo.
"Ni kweli leo asubuhi Haruna (Niyonzima) tumemfanyia upasuaji mdogo wa kipele kwenye pua yake katika hospitali ya Mwananyamala."
"Kipele hicho kilimtokea kwenye pua yake. Hakikuwa sehemu nzuri, kwa hiyo tumelazimika kumfanyia upasuaji huo mdogo."
"Kidonda hicho hakiwezi kuathiri utendaji wake wa kazi. Kesho (leo) ataendelea na mazoezi kama kawaida na wenzake kujiwinda na mchezo wa JKT Ruvu." alisema Matuzya.
Alisema kidonda cha upasuaji huo kitakuwa kimepona mara baada ya saa 48 ambazo ni sawa na siku mbili.
"Hadi kufika Jumapili atakuwa hana tatizo lolote. Nafikiri suala la kucheza linabaki kwa mwalimu wa timu." alisema daktari huyo.
SOURCE SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment