Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 4, 2013

PICHA ZA RAMANI YA UJENZI WA UWANJA WA YANGA, HIVI NDO UTAVYOKUA




Ramani ya uwanja mpya wa klabu ya Yanga - Kaunda Stadium unavyoekana kwa ndani

Kampuni ya Beinjing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi akinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi akinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.
Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.
Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000.
Katika uwasilishaji huo wa makadirio ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa kukamilisha zoezi la upembuzi akinfu mapema ambapo leo wamepata fursa ya kujionea na kujua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.


Ramani ya mchoro wa Uwanja mpya wa Kaunda unavyoonekana kwa nje

Kufukwe alisema wamepewa nafasi ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mktaba kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda.

Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za ujenzi wa uwanja, Kufukwe alisema ujenzi wa uwanja wa mpya utajengwa na wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.

Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maaalumu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.
 SOURCE:http://www.youngafricans.co.tz

No comments:

Post a Comment