Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Linus Sinzumwa akitoa taarifa
ya tukio la kukamata bunduki ya kijeshi SMG kwa waandishi wa habari
(hawapo kwenye picha). Bunduki hiyo inayodhaniwa kutumika kwenye matukio
ya uhalifu, imekamatwa katika kijiji cha Mwamangembe jimbo la Manyoni
magharibi.
Afisa
upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka
(wa kwanza kulia) akifuatilia taarifa ya kukamatwa kwa bunduki ya
kijeshi aina ya SMG iliyokuwa ikitolewa na kamanda wa polisi mkoa wa
Singida,Linus Sinzumwa.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Jeshi
la polisi mkoani Singida, limefanikiwa kukamata bunduki ya kijeshi aina
ya SMG na risasi zake 28, inayodhaniwa kuwa hutumika katika matukio ya
uhalifu.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa amesema bunduki hiyo
wameikamata Aprili saba saa saba usiku katika kijiji cha Mwamangembe
tarafa ya Itigi jimbo la Manyoni magharibi.
No comments:
Post a Comment