Kamanda
wa polisi Mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimek akizishika nyara za serikali
hizo ambazo zimekamatwa(mikia ya tembo) Kwa hisani ya http://demashonews.blogspot.com
Jeshi
la Polisi mkoani Ruvuma katika wilaya ya Tunduru kijiji cha Mbalikiwa
kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga linamshikilia kijana ambaye
anafahamika kwa jina la Bakari Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni
mkazi wa eneo hilo kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali.
Kamanda
wa polisi mkoani Ruvuma Deusidedit Nsimeki ameyasema hayo jana mapema
wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumla ya mikia
ya Tembo 10 imekamatwa na askari ambao walikuwa doria katika eneo la
Mbalikiwa Febriari 5/2013 majira ya saa:7 usiku, jumla ya idadi hiyo ya
mikia ni sawa na idadi ya Tembo 10 waliouwawa na idadi ya meno ni 20
yenye jumla ya dola za kimarekani elfu 15 sawa na zaidi ya milioni 245
kwa fedha za kitanzania
Mtuhumiwa
Bakari Said jana amefikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kujihusisha na
biashara haramu ya nyara za serikali ambapo taarifa za tukio hilo la
uhalifu zilipatikana kutoka kwa raia wema pia kamanda wa polisi
aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wao wa dhati hili kwa
jeshi la polisi ili kuweza kudhibiti kabisa huarifu huo.
No comments:
Post a Comment