Kiukweli inasikitisha sana kwa Madaktari wa HOSPITALI YA GENERAL iliyoko mjini Dodoma kutomtibu mtoto Ombeni Mbeula kwa takribani miezi miwili kwa ukosefu wa pesa kutoka kwa familia yake. Isitoshe mtoto mwenyewe ana miaka mitano (5) inabidi kiutaratibu apate matibabu bure, hivi kweli uongozi wa hospitali ya General umelisimamiaje jambo hili?. Kiukweli inasikitisha kwa madaktari kutomjali mtoto Ombeni Mbeula mpaka habari iliporushwa kwenye mtandao na washiriki wake wa blog nyingine ndipo madaktari walipoanza kuitwa lakini hawajaenda kumtibu mtoto huyo.
Kwa moyo wa dhati tunawashukuru wale wote waliotoa michango yao kupitia kupitia kwenye namba ya ndugu yake ambayo ni Ekiria Paskali na namba yake ya simu ni 0757 498336
Hawa ni baadhi ya wale walioguswa na tukio hilo na kutoa mchango wao wa hali na mali
jumla ya michango ni shilingi 421,300 mpaka naondoka hospitalini hapo kuna watu walikuwa bado wanaendelea kuchangia. Kama ulikuwa unataka kumchangia mtoto huyu apate matibabu tuma mchango wako kwa kutumia namba hii 0757 498336 mwenye jina lake ni Ekiria Paskali
No comments:
Post a Comment