Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, May 27, 2013

ANGALIA PICHA ZA OMBAOMBA ANAYETAPELI WATU KWA KUIGIZA HANA MKONO MMOJA NA MGUU ACHEZEA KICHAPO AONYESHA MIKONO YOTE NA MIGUU


Omba omba tapeli anayejifanya hana  mikono akikamatwa na  wananchi  baada ya  kukimbia
Hapa  akibanwa  kuonyesha  mikono yake  yote  miwili
Wananchi eneo la Miyomboni  wakiwa  wamembana omba omba  huyu tapeli kuonyesha  mikono yake  yote

'' Huwa  unasema wewe  ni  mlemavu  huna mkono mmoja   hii nini ....nyosha  juu  watu waone utapeli  wako"
Hapa  kipigo  kilipoanza  kwa  mzee  huyo tapeli  anayejifanya  hana  mkono  mmoja na mguu
Hapa  ni  kipigo  kikiendelea

Tapeli  huyo akitaka  kujinasua  kutoka  mikono ya  wananchi  wenye hasira  kali
Hapa  baada ya  kupata upenyo akivaa nguo  zake
Hapa  akiwa ameachiwa  na kuanza kutimua mbio

Baada ya  kuchezea kichapo  tapeli huyo  sasa anajaribu  kuficha aibu

OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO

Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo

Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo

 

AMA Kweli  mwisho  wa  utapeli ni aibu  kubwa na   wahenga walinena   kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo kwa  wakazi  wa Miyomboni mjini Iringa wamepata  kushuhudia  kituko cha mwaka  baada ya watu  waliochoka  kuvumilia vitendo vya  kitapeli  vinavyofanywa mzee  mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
 
Tapeli  huyo  mbali ya  kuumbuliwa kwa  kutakiwa  kuonyesha miguu  yake  yote  pamoja na mikono  yake  yote  bado amepata  kuchezea  kichapo  kiasi cha  kunusurika  kuuwawa na wananchi  hao wenye hasira  kali.
  ndio ulipata  kufichua siri  hiyo ya omba omba  huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano  wa mlemavu .
 
Kutokana na kufichuliwa kwa  siri  hiyo ya  kujiigiza  kuwa ni  omba omba mlemavu wananchi wamekuwa  wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na  kumtimua  mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua  kumkimbiza  kutoka eneo la Hazina  Ndogo  hadi miyomboni na kuanza  kumpa  kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo  vyote kuwa  si mlemavu
 
Tapeli  huyo mbali ya  kujifanya ni mlemavu  wa  viungo  wakati mwingine huwa anajifanya  ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama  mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu  mmoja na  kuwaomba  watu fedha za matibabu .

Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)

Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  kutokana na  kichapo alichokipata  na kuumizwa  vibaya usoni .
 
Hata  hivyo  inasemekana  mzee  huyo  amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali  mbali kutokana na mbinu yake ya  kufuru anayoifanya  kuwa ni mlemavu  wakati si mlemavu na  kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya  kiuchumi kuliko  kuwaigiza  walemavu na  kuwa iwapo atarudia na  kukutwa akifanya  hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema  wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya  hivyo .
 
Aidha  anadaiwa chanzo cha  kichapo  cha  leo kwa mzee  huyo tapeli ni mmoja kati ya  mpenzi  wake ambae  alikuwa amemsusa na  kuhamia kwa mpenzi mwingine  kuueleza umma kuwa  huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi  wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea  wananchi kufanya udadisi .
 
Kabla kufukuzwa na kuchezea  kichapo tapeli huyo alifukuzwa  eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya  vijana  wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona  viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
 
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada. CHANZO FRANCIS GODWIN

No comments:

Post a Comment