Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo
kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio
na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua
aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.Sheha huyo alimwagiwa
tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji
na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza
kumtambua.
Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa MnazoMmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo. |
No comments:
Post a Comment