CHAMA cha
CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali kuomba radhi kutokana na
vurugu zilizosababishwa na CUF yenye mrengo wa Kiliberali na Chadema
imemafanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na
usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati
ya Maadili ya Bunge kufanya kikao kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa
2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi na pia
kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi;
kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje
wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa
Kiliberali ambazo pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF,
Rashidi wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema
kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” amesema hivi punde Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesimama Bungeni hivi pinde na kuwaomba
radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni
jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo,
Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema
kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni
shoga na usagaji na kwamba hawakufanya kosa, pia alisema CUF
alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na
kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali wamelifanya leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati
hiyo John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki
amesema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa
mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama
za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi
mkono masuala hayo.
No comments:
Post a Comment