Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 24, 2013

DAKTARI WA MENO KITUO CHA AFYA SABASABA AJINYONGA NA KUFA NDANI YA GESTI MOROGORO



MWILI wa Dk Anold Limo ukiwa katika chumba cha kuifadhia maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kuondolea katika nyumba ya kulala wageni ya Camel Nkomola Kihonda baada ya uchun
guzi katika hospitali ya mkoa huo mei 22 mwaka huu.
DAKTARI wa meno Anorld Rimo (umri wa miaka kati ya 30 hadi 40) wa hospitali ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro, amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya Camel iliopo Kihonda.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 10 alfajiri katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
Alisema Daktari huyo alikuwa amepanga katika nyumba hiyo katika chumba namba 2, na kukutwa amejinyongea dirishani kwa kutumia foronya za mto pamoja na taulo. Ameeleza kuwa usiku wa kuamikia siku hiyo marehemu alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo  na kufanya fujo na kuonesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi kazi.
Kamanda huyo alisema marahemu alikuwa peke yake katika chumba hicho na haikufahamika mara moja anaishi wapi.

Chanzo cha kujinyonga hakijajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi.

No comments:

Post a Comment