Mradi
wa kuwapatia wanafunzi wa Skuli ya Kusini iliyopo Makunduchi waanza
rasmi kwa majaribio jana. Akizinduwa rasmi mradi huo mwakilishi wa Mkuu
wa Wilaya ya Kusini, ndugu Faida Khamis Ali (wa tatu kutoka kushoto)
aliwataka uongozi wa Skuli ya Kusini kuuenzi mradi huo kwa kutumia fedha
za wafadhili kama zilivyokusudiwa.
Wakati
huo huo mratibu wa mradi huo ndugu Mohamed Muombwa ambaye pia ni
msaidizi wa Makamo wa pili wa rais, amesema mradi huo unaofadhiliwa na
skuli rafiki Sundsvalls Gymnasium kutoka Sweden utawapatia chakula cha
mchana wanafunzi wote 1000 kutoka msingi na sekondari.
Alisema
kwa kuanzia chakula hicho kitatolewa wiki mara moja kwa kipindi cha
mwezi mmoja. Malengo ya baadaye ni kuwapatia wanafunzi chakula cha
mchana kwa siku zote 5.
Jumla ya
shillingi 1.3 milioni zilitumika kugharamia mlo huo wa mchana. Kati ya
fedha hizo shillingi 600,000 zilitumika kununua ng'ombe kwa ajili ya
kitoweo.
No comments:
Post a Comment