Diwani wa kata hiyo ya Kwakilosa Hamza Ginga akiwa ameshika mkoba wa mjane huyo uliopotea pamoja na madaftari ya watoto kimiujiza |
Hili ni paa la nyumba hiyo inayoungua kimiujiza kwa zaidi ya mara tano sasa kama inavyoonekana ikiwa salama salimini |
Mwanamke Bi. Faraja Chengula (31) na watoto wake akiwa na familia yake pamoja na diwani wa kata ya Kwakilosa mheshimiwa Hamza Ginga na baadhi ya viongozi wa mtaa huo wa Beila baada ya mali katika nyumba yake kuteketea kwa moto wa miujiza .
Mjane Bi Faraja Chengula
........................................... HUJAFA hujaumbika bado ni kauli ya mwanamke mkazi wa mtaa wa Beila kata ya Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa Bi. Faraja Chengula (31) ambae amelazimika kuikimbia nyumba aliyopanga na kwenda kuomba hifadhi kwa kiongozi mmoja wa kidini kama njia ya kujinusuru na mauza uza haya moto kimiujiza umeendelea kumtesa kwa kuteketeza mali mbali mbali bila kuleta madhara kwa binadamu.
Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo
mwanamke huyo ambae ni mjane aliyepoteza mwenzi wake kwa zaidi ya miaka
mitatu sasa alisema kuwa mauza uza hayo ndani ya chumba chake yalianza
toka jumatano ya April 17 mwaka huu baada ya kurejea nyumbani na kupatwa
na wakati mgumu kutafuta ufunguo wa nyumba ambao ulipotea katika
mazingira tata.
Bi.
Chengula alisema kuwa mbali ya kupotea ufunguo huo bado aliendelea
kushuhudia mauza uza mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuibuka kwa moto
ambao chanzo chake bado kufahamika na mbaya zaidi moto huo ulikuwa
unawake katika kitanda bila kuteketeza godoro na baada ya kuuzima kwa
maji bado uliibuka moto mwingine katika mito ya makochi aliyokuwa
ameiweka nje ya chumba hiyo.
“
Kweli nashindwa kuelezea ila nilishangazwa zaidi baada ya kuona mito
hiyo ya makochi iliyokuwa nje ya chumba ghafla ikiwa ndani ya chumba na
kuwaka moto huku nikishuhudia moto huo ukishika kasi na hata
nilipojaribu kuzima kwa maji ilishindikana “
Hata
hivyo alisema kuwa hadi sasa bado hajatambua miujiza hiyo inatokana na
nini kwani toka mume wake amefariki dunia ni zaidi ya miaka miwili sasa
na hakuna jambo lolote kama hilo ambalo limepata kujitokeza na kuwa
mbaya zaidi mazingira ya moto huo yamekuwa wakimshangaza kila mkazi wa
nyumba hiyo yenye wapangaji zaidi ya 10 pamoja na majirani wanaozunguka
nyumba hiyo.
Bi.Chengula
alisema kuwa wakati mwingine amekuwa akizikuta nguo zake na za watoto
wake wawili chooni na baada ya kurejea ndani ya chumba hicho amekuwa
akizikuta zikiwa ndani na mara nyingine moto huo umekuwa ukiwaka katika
eneo la sokte ya umeme bila sokte hiyo ya plastick kuguswa na moto huo .
“Kweli
nashindwa kujua chanzo cha mambo haya kwa sijala kituo cha mtu yeyote
na mimi ni mlokole ninayesali kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) usharika wa Mlandege na mbali ya kufanya maombi kanisani ila bado
mambo haya yameendelea kuniandama na zaidi ya mara tano sasa moto
unawake ndani ya chumba changu pekee “
Aidha
alisema kutokana na mauza uza hayo kuchukua kasi alilazimika kuwaita
waumini wenzake na kufanya maombi katika chumba hicho ila wakati
wakiendelea kufanya maombi ghafla walijikuta simu za viganjani zikiwa
zimepotea katika mazingira yenye utata na hadi sasa simu hizo
hazijapatikana.
Pia
alisema kuwa juzi katika mazingira tata madaftari ya wanafunzi
yaliyokuwa katika mfuko ,mkoba wake wa mkononi uliokuwa na vitu mbali
mbali pamoja na pea moja ya viatu vyake vilipotea katika mazingira tata
ila leo April 26 majiar ya saa 2 asubuhi baada ya viongozi wa serikali
ya mtaa na diwani kufika eneo hilo wakiwa na mwandishi wa habari hizi
vitu hivyo vilionekana eneo ambalo ni jeupe sana pamoja na kuwepo kwa
umande katika eneo hilo ila vitu hivyo havikugusa hata tone la umande.
Balozi
wa mtaa huo wa Beila Bi. Christina Ndale alisema kuwa nyumba hiyo
ambayo imekuwa ikiandamwa na mauza uza hayo ni nyumba Block ‘Y’79 na
kuwa wao kama mtaa wamepata kushuhudia mauza uza hayo nab ado wanaumiza
vichwa kujua chanzo cha mambo hayo .
Wakati
mwenyekiti wa mtaa huyo Alan Koma koma alisema kuwa mauza uza kama hayo
si mara ya kwanza kujitokeza katika mtaa huo kwani kwa upande wake pia
mambo kama hayo yalipata kumtokea kwa nyumba yake kupigwa mawe usiku
kucha na watu wasiofahamika mbali ya kulindwa na askari polisi na
wananchi kuzunguka nyumba hiyo kwa ulinzi wa sungusungu ila bado mawe
hayo ambayo yalikuwa yakimwagika kama mvua kutoka angani yaliendelea
kushambulia nyumba hiyo .
Hivyo
alisema suala hilo la mauza uza ni miongoni mwa mambo ambayo yanawatesa
wakazi wa eneo hilo hivyo kuwaomba watu wanaojihusisha na imani za
kishirikina kwa ajili ya kuwatesa wengine kuachana na masuala hayo.
Diwani
wa kata ya Kwakilossa mheshimiwa Hamza Ginga akithibitisha kutokea kwa
matukio hayo alisema kuwa yeye kama diwani anashindwa kujua sababu kuu
ya mambo hayo japo ana mpango wa kuitisha mkutano ili kukutana na
wananchi wake wote kama njia ya kumaliza mauza uza hayo.
Mheshimiwa
Ginga alisema kwa sasa wanakusudia kuwaita viongozi wa dini waliopo
mjini Iringa kutoka nchini Kenya , Uganda na mwenyeji wao askofu wa
kituo cha maombezi na uponyaji cha Overcomers Power Center Dkt Boaz
Sollo ali kufanya maombi maalum katika nyumba hiyo na kumtaka mwamake
huyo kutoukimbia mtaa kutokana na mauza uza hayo kwani hata kama atahama
kama kuna mtu anamfuatilia ataendelea kufanya hivyo.
MWISHO
Credits: Matukiodaima Blog
|
No comments:
Post a Comment