SIFA KUBWA: David Beckham aliungana na watoto wake kushangilia ubingwa ligi ya Ufaransa ambapo amewasaidia PSG kutwaa ndoo hiyo.
Baada ya kutolewa uwanjani hapo jana, Beckham alionekana akiwa hivyo
MACHOZI
YAKIMTOKA: David Beckham alitokwa na machozi baada ya kuona kocha wake
Carlo Ancelotti anataka kumtoa uwanjani ili kumpisha mchezaji mwingine
MCHEZO WA MWISHO: David Beckham alicheza mexhi yake ya mwisho akiwa na PSG dhidi ya Brest hapo jana
Wachezaji wa PSG wakimkumbatia Beckham baada ya kufanyiwa mabadiliko
DAVID
BECKHAM alitoka Uwanjani katika Mechi yake ya mwisho ya Nyumbani ya
Klabu yake Paris St-Germain ambayo huenda ikawa ndio ya mwisho katika
maisha yake ya Soka ya Miaka 20 huku akibubujikwa machozi.
Beckham,
ambae alianza Mechi hiyo ya Ligi dhidi ya Brest kama Nahodha,
alibadilishwa katika Dakika ya 81 na Mechi kusimama kwa muda huku
Wachezaji wenzake wa PSG wakimshangilia na yeye akawa akitoka nje kwa
machozi.
Mashabiki wengi wa PSG wamekuwa wakililia Beckham, Miaka 38, abakie kama Mchezaji badala ya kustaafu.
Msimu
huu PSG ndio wamekuwa Mabingwa wa France na bado wana Mechi moja ya
Ligi Jumapili ijayo watakayocheza Ugenini na Lorient lakini inaaminika
Beckham hatakuwepo.
Katika
Mechi ya Jana PSG waliifunga Brest Bao 3-1 huku Beckham akitengeneza
Bao moja kwa Kona yake kuunganishwa na Blaise Matuidi na Bao nyingine
mbili kufungwa na Zlatan Ibrahimovic.
Bao la Brest lilifungwa na Charlison Benschop.
Mara
baada ya Filimbi ya mwisho kwenye Mechi hiyo na Brest, Beckham
aliwahutubia Mashabiki na kusema: “Nataka kumshukuru kila Mtu hapa
Paris-Wachezaji wenzangu, Wafanyakazi na Mashabiki. Ni kitu kikubwa
kumalizia Soka langu hapa. Nimemaliza Soka nikiwa Bingwa na kwenye Timu
iliyonifanya nijione kama nimekaa Miaka 10!”
Wachezaji
wa PSG walimbeba na kumrusharusha juu huku akishuhudia na Mkewe
Victoria na Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.
No comments:
Post a Comment