Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, May 13, 2013

PICHA ZA DK. KAFUMU AFUNIKA IGUNGA ALIVYOPOKELEWA.


4
Mbunge wa jimbo la Igunga aliyerejeshwa na mahakama kuu Dk Peter Kafumu akizungumza na wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini humo leo kuwashukuru wananchi na wapiga kura wake kwa kuwa naye bega kwa bega katika matatizo hayo, Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga ukiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri kuu ya CCM Ndugu Nape Nnauye, amesema anaomba ushirikiano kwa kila mwana Iguna bila kujali itikadi za vyama vya siasa. 
 5
Mbuge wa Jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu akihutubia mkutano wa hadhari mjini Igunga leo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi NEC 6
Maelefu ya wana Igunga wakiwa katika mkutano huo leo



Wananchi wa Igunga wakipmokea  mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe wa kumkaribisha jimboni mwake
 3
Dk Peter Kafumu akivishwa shada la maua mara baada ya kuwasili mjini Igunga

Mbunge wa Igunda, Dk. Peter Dalally Kafumu akiwasalimia wananchi katika mkutano wa mapokezi yake uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga mkoani Tabora. Kuliani Katibu wa NEN, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye.(Picha na Bashir Nkoromo)
NA BASHIR NKOROMO,IGUNGA
WAKATI mapokezi ya Mbunge wa Igunga Dk. Dalally Peter Kafumu yamesababisha baadhi ya shughuli kusimama, kwa hoi hoi, nderemo na 
vifijo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi ilizotoa katika jimbo hilo. 
Akizungumza kwenye mkutano wa mapokezi ya Dk. Kafumu uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM lazima itazitekeleza ahadi zote zilizotolewa na mbunge huyo kupitia ilani ya Chama wakapi akigombea katika uchaguzi mdogo uliofanyika 2011 jimboni humo.
“Baada ya mahakama kumrejeshea Ubunge mbunge wetu, CCM inaahidi kwamba ahadi zote alizotoa mbunge wenu zitatekelezwa kabla ya mwaka 2015. Na kwa kuwa Chadema walipunguza kasi kwa kusimamisha mbunge wenu baada ya kumpeleka mahakamani, CCM itaisimamia serikali ili kuhakikisha inaongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi hizo kufidia pale utekelezaji ulipokuwa umepungua kasi”, alisema Nape.

No comments:

Post a Comment