Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 16, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE ANA KWA ANA NA WABUNGE WA CCM


 
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya kikao cha siku mbili na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujadili masuala mbalimbali ya taifa, ikiwamo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika majimbo yao.
Katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, anatarajiwa kuwapa nguvu wabunge wake katika kueleza masuala mbalimbali, ikiwamo hatua ya Serikali kupitisha bajeti, huku miradi ya maendeleo ikisuasua katika utekelezaji kwa madai ya kukosekana kwa fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kikao hicho ni cha kazi na kitakuwa kinatoa nafasi zaidi kwa wabunge kueleza masuala yanayoh
usu utekelezaji wa Ilani ya CCM katika majimbo yao.
Nape alisema kikao hicho hakina uhusiano wa aina yoyote na matukio yanatokea bungeni hivi sasa, bali ni ratiba ya kikao cha kazi za Mwenyekiti katika kupima utekelezaji wa ilani na miradi ya maendeleo katika majimbo mbalimbali ambayo yapo chini ya wabunge wa CCM.
“Hiki ni kikao cha kazi, ninapenda kueleweka kuwa CCM ndiyo iliyokabidhiwa jukumu la kuongoza nchi hii na wabunge wa chama chetu ndiyo wanaisimamia ndani ya Bunge, hasa katika kuhoji masuala mbalimbali yanayohusu nchi na watu wake. 
“Lakini kutokana na hali hii, kikao hiki kitakuwa cha siku mbili ambako siku ya kwanza itakuwa ni fursa kwa wabunge kusema masuala mbalimbali dhidi ya serikali yao.

No comments:

Post a Comment