Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego
mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye
namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya
kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo
ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano
ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya
Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili
ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki
risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa
na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa
majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika,
Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja
ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito
kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao
ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment